Ili kutusaidia kutambua upendo mkuu wa Mungu, Yesu alitupa mfano wa mwana mpotevu katika Injili ya Luka. Mtu mmoja alikuwa na wana wawili. Mwana mdogo akamwambia baba yake, “Baba, nipe sehemu ya mali inayonistahili.” Basi baba akawagawia mali yake.
Mwana mdogo akakusanya vitu vyake vyote na kusafiri kwenda nchi ya mbali, ambako akaitapanya mali yake kwa maisha ya anasa. Njaa kali ikatokea katika nchi hiyo naye akawa maskini. Hatimaye akaajiriwa na mtu wa nchi hiyo na kupelekwa mashambani kulisha nguruwe. Alitamani kujishibisha kwa maganda yaliyokuwa yakiliwa na nguruwe, lakini hakuna mtu aliyempa chakula.
Akajirudia na kusema, “Ni watumishi wangapi walioajiriwa na baba yangu wana chakula cha kutosha, nami hapa ninakufa kwa njaa! Nitaondoka niende kwa baba yangu, nimwambie, ‘Baba, nimetenda dhambi juu ya mbingu na mbele yako; sistahili tena kuitwa mwanao; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.’”
Akaondoka akaenda kwa baba yake. Baba yake alikuwa akimngojea mwana aliyekuwa ameondoka nyumbani kwenye lango kila siku. Mwana alipokuwa bado mbali, baba yake alimwona, akamhurumia, akakimbia na kumkumbatia na kumbusu. Baba alifurahi sana, akawaambia watumwa wake wamletee joho bora na kumvisha, amtie pete mkononi na viatu miguuni, kisha walete ndama aliyenona wamchinje na kufanya karamu ya kusherehekea kurudi kwa mwanawe.
Vivyo hivyo, haidhuru tumetenda dhambi za aina gani; tukizitubia kweli na kuziacha, Mungu Baba yetu hutusamehe na kutukumbatia. Kama baba alivyomvisha mwana mpotevu joho bora, Mungu husafisha mioyo yetu kwa damu ya Yesu Kristo na kutuvika kitani safi ili tuweze kuingia mbinguni. Kama baba alivyompa pete mwanawe aliyerudi nyumbani, Mungu hutuahidi wokovu na uzima wa milele, na hutupa majibu na baraka zisizo na kikomo tunapoamini Neno lake na kulitii.
Baba kuwaambia watumwa wake walete ndama aliyenona, wamchinje, wale na kusherehekea kurudi kwa mwana kunamaanisha kwamba Mungu hutupa chakula cha kiroho. Vivyo hivyo, tunapochoka na kuvunjika moyo duniani, tukirudi kwa Mungu kama mwana mpotevu, wema wake humfanya atukaribishe, atupe chakula cha kiroho kikamilifu na kutuweka katika amani. Ninaomba kila mmoja wenu amkabidhi Yesu Kristo mizigo yote ya maisha yake na afurahie amani ya kweli ndani ya Mungu. Ninaomba haya katika jina la Bwana wetu!
His Emeritus Bishop Dr. Jaerock Lee
Leo, majanga na matatizo mbalimbali yanaikumba dunia nzima. Tishio la silaha za nyuklia za Korea Kaskazini, uchafuzi wa hewa na maji,
Mfalme na maafisa wake walimwacha Mungu na kuabudu sanamu. Ghadhabu ya Mungu ikawajia watu wa Yuda, nao wakavamiwa na jeshi la Waaramu.
Upendo hautafuti faida yake mwenyewe, bali hujitoa kwa ajili ya wengine. Huo ndio upendo wa kweli wa kiroho usiobadilika milele. Mungu anataka tuishi katika wema na haki, na kuitimiza Sheria kwa upendo.